Msemo “Ramadhaan Kariym” kwa mtazamo wa al-Fawzaan

Swali: Kusema kusema “Ramadhaan Kariym”, Ramadhaan yenye kutoa, je mtoaji si ni Allaah?

Jibu: Hili halina msingi. Kusema “Ramadhaan Kariym”, Ramadhaan yenye kutoa, hili halina msingi. Ama kusema Ramadhaan tukufu (شريف), iliyobarikiwa (مبارك) na tukufu (عظيم), sifa hizi zimepokelewa katika Hadiyth. Hakuna ubaya. Lakini “Kariym” sijui msingi wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/node/%2013425
  • Imechapishwa: 08/05/2022