Kupwekesha jumamosi na ijumaa kwa anayefunga swawm ya Daawuud

Swali: Mimi ni kijana ambaye alikuwa mwenye kuchunga swawm ya Daawuud (´alayhis-Salaam). Lakini nimepata wenye kunambia kuwa swawm yangu ikikutana na jumamosi au ijumaa basi nisipwekeshe siku hizo kwa funga. Wamesema kuwa haya ni maoni ya Shaykh al-Albaaniy (Hafidhwahu Allaah). Nimebaki ni mwenye kufunga katika hali ya kuchanganyikiwa. Nataraji kupewa faida hukumu ya kufunga jumamosi na ijumaa peke yake ikiwa mtu anafunga swawm ya Daawuud, ikikutana na siku ya ´Arafah au ´Aashuuraa´?

Jibu: Anayefunga swawm ya Daawuud (´alayhis-Salaam) basi hapana vibaya kwake kufunga siku ya ijumaa au siku ya jumamosi siku hizo zikukutana na funga yake anayofunga. Vivyo hivyo hakuna kikwazo cha kuzifunga zikikutana na siku ya ´Arafah au siku ya ´Aashuuraa´. Kwa kuongezea ni kwamba Hadiyth kusudiwa inayokataza kufunga jumamosi peke yake sio Swahiyh.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/314) nr. (17600)
  • Imechapishwa: 08/05/2022