Ni lazima swawm ya Shawwaal ianze tarehe 2 Shawwaal?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kuwa swawm ya siku sita za Shawwaal ni lazima ianze siku ya pili ya mwezi huu na khaswa kwa wale wazee?

Jibu: Swawm ya siku sita za Shawwaal ni yenye wasaa katika kila mwezi; mwanzoni mwake, katikati yake au mwishoni mwake. Ni mamoja kwa kufuatanisha au kwa kuachanisha. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia [siku] sita za Shawwaal, basi anakuwa kama amefunga mwaka mzima.”[1]

Kwa hivyo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufunga siku sita za Shawwaal kwa kuachia katika Shawwaal yote.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Bakr Abu Zayd

[1] Muslim (1164).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/304) (16374)
  • Imechapishwa: 08/05/2022