Kuchinja baada ya kumaliza siku sita za Shawwaal

Swali: Je, baada ya kumaliza kufunga siku sita za Shawwaal kunachinjwa kichinjwa au kuna sherehe? Nimewasikia baadhi ya watu wakisema kuwa ni lazima kuchinja.

Jibu: Kufunga siku sita za Shawwaal ni kitu kimependekezwa. Baada ya kuimaliza haikusuniwa kuchinja wala kufanya kitu kingine.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (16730)
  • Imechapishwa: 08/05/2022