Mwanamke kufunga sunnah bila idhini ya mume wake

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kufunga bila idhini ya mume wake mwezi usiokuwa Ramadhaan?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kufunga pasi na idhini ya mumewe. Hilo ni kutokana na yale aliyopokea Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke asifunge na mume wake yuko [hakusafiri] isipokuwa kwa idhini yake.”[1]

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) pia ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke asifunge siku na mume wake yuko [hakusafiri] mbali na mwezi wa Ramadhaan isipokuwa kwa idhini yake.”[2]

Kutokana na hayo haifai kwa mwanamke kufunga swawm iliyopendekezwa isipokuwa kwa idhini yake. Kwa sababu swawm iliyopendekezwa ni Sunnah na haki ya mume ni wajibu. Kufunga kutamzuilia kutokamana na baadhi ya haki zake za wajibu juu yake mke.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

[1] al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake. Tazama ”Fath-ul-Baariy” (09/293).

[2] Abu Daawuud katika ”as-Sunan” yake. Tazama ”´Awn-ul-Ma´abuud” (07/128) na Ibn Maajah katika “as-Sunan” yake (01/56).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (19307)
  • Imechapishwa: 08/05/2022