Msafiri kusubiri na kujiunga na imamu katika Rak´ah mbili za mwisho

Swali: Baadhi ya wasafiri wanaingia misikitini na wanakuta kuna Jamaa´ah inayotaka kusimamishwa. Wanasubiri mpaka imamu aswali Rak´ah mbili ikiwa ni swalah ya Rak´ah nne kisha wanajiunga naye katika Rak´ah mbili za mwisho kwa hoja ya kwamba wao ni wasafiri wanafupisha.

Jibu: Hili si sawa, haijuzu na swalah zao hazisihi. Wanachotakiwa ni kuingia pamoja na imamu na kuswali kikamilifu swalah zao. Kwa kuwa hukumu zao ni hukumu za Imamu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Imamu amewekwa ili afuatwe.”

Msafiri akiswali nyuma ya mkazi anachotakiwa ni kuswali kikamilifu swalah zake. Lakini kusubiri mpaka kunapobaki Rak´ah mbili, ni nani aliewatolea fatwa hii? Huu ni ujinga na haijuzu. Swalah zao hazisihi kwa kuwa hukumu yao ni hukumu ya Imamu. Imamu anaswali kikamilifu hivyo na wao wanalazimika kuswali kikamilifu.

Hata kama hawakuwahi pamoja na Imamu isipokuwa Tashahhud ya mwisho, wanalazimika kuswali kikamilifu. Kwa kuwa hukumu yao ni hukumu ya Imamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo-01-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 03/05/2015