Msafiri kukusanya na kufupisha kabla ya kuacha mji wake

Swali: Wakati mwingine msafiri anafanya makisidio kuwa atafika katika mji wake katika swalah ya ´Ishaa.

Jibu: Ni sawa akiiswali safarini. Akiswali katika hali hiyo basi ataswali Rak´ah mbili. Na akisubiri mpaka atakapofika katika mji wake ataiswali Rak´ah nne.

Swali: Wakati mwingine wakati wanapofika katika vituo vya mafuta kabla ya kufikisha 80 km au chini ya 80 km wanaswali Maghrib pamoja na ´Ishaa kwa kukusanya na kufupisha.

Ibn Baaz: Ni wasafiri?

Muulizaji: Ndio.

Ibn Baaz: Hapana vibaya.

Muulizaji: 80 km?

Ibn Baaz: Hapana neno wakiswali kabla ya kufika katika mji wao. Kwa msemo mwingine wakiuacha mji wao.

Muulizaji: Hapana, ni kabla ya kuacha mji wao.

Ibn Baaz: Hapana. Kama hivo wataswali Rak´ah nne. Wakiacha miji yao ndio wataswali Rak´ah nne. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapoacha Madiynah ndipo anaswali Rak´ah mbili Dhul-Hulayfah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23075/حكم-الجمع-والقصر-للمسافر-قبل-الوصول-للبلد
  • Imechapishwa: 02/11/2023