Machukizo ya kulala na janaba bila kuoga

Swali: Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) inasema kuwa wakati mwingine Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa analala akiwa na janaba na hagusi maji. Ni Swahiyh?

Jibu: Wameitia kasoro. Ina kasoro. Ni miongoni mwa mapokezi ya Abu Ishaaq as-Subay´iy na hakusema wazi amesimulia kutoka kwa nani. Kinachotambulika kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kumjamii mke wake alikuwa akitawadha, akioga, akiosha dhakari yake, akitawadha na akilala. Wakati mwingine akitanguliza kuoga. Hakuwa akilala isipokuwa baada ya kutawadha, kama alivyomwambia ´Umar:

“Tawadha, kisha ndio ulale.”

Hapo ilikuwa pale ´Umar alipomwambia:

“Ee Mtume wa Allaah! Nilale nikiwa na janaba?” Akamjibu:

“Hapana, tawadha, kisha ndio ulale.”

Imekuja katika tamko jengine:

“Atawadhe na alale.”

Swali: Vipi ikiwa hatotawadha?

Jibu: Inachukiza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Machukizo ya kulala na janaba bila kuoga
  • Imechapishwa: 02/11/2023