Kusoma kwa sauti ya juu katika swalah inayopendeza mchana

Swali: Je, inafaa kwa mtu anayeswali swalah inayopendeza kunyanyua sauti yake ndani yake?

Jibu: Ndio, katika swalah ya usiku.

Swali: Mchana?

Jibu: Hapana, Sunnah ni kusoma kimyakimya. Swalah ya mchana asome kimyakimya. Isipokuwa tu swalah ya Fajr na swalah ya ijumaa.

Swali: Anataka kufanya marejeleo ya Qur-aan.

Jibu: Hapana. Sunnah ni kusoma kimyakimya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma kimyakimya katika swalah zinazopendeza za mchana.

Swali: Je, inafaa kwake kusoma kwa sauti ya juu akiswali na mwingine swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Hapana, Sunnah ni yeye kusoma kimyakimya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23074/حكم-رفع-الصوت-وخفضه-في-النوافل
  • Imechapishwa: 02/11/2023