Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayesikia adhaana na asiitikie basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.”[1]

Je, hili linahusu katika hali ya wenyeji au ni yenye kuenea mjini na safarini?

Jibu: Ni kwa wenyeji. Wasafiri wana ruhusa ya kuswali wenyewe. Isipokuwa akiwa mtu mmoja. Katika hali hiyo atalazimika kuswali na mkusanyiko. Kuhusu wasafiri haiwalazimu kuswali na wanaoswali kwa kukamilisha. Isipokuwa akiwa mmoja atalazimika.

[1] Ibn Maajah (785).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22121/حكم-صلاة-الجماعة-في-الحضر-والسفر
  • Imechapishwa: 27/10/2022