Swali: Je, inafaa kwa timu mbili za mpira wa miguu kuchezea tuzo ikiwa tuzo hiyo inadhaminiwa na chama cha nje?

Jibu: Haijuzu kuchezea tuzo hata kama imefadhiliwa na watu wa nje. Haijuzu kuchezea kitu katika mazoezi kama haya. Hata hivyo ni halali ikiwa hakuna maasi na mambo yanayokwenda kinyume, kwa sababu ni mazuri kwa mwili, lakini yasichezwi kwa tuzo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 05/03/2022