Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkimsikia yeyote anatangaza msikitini mnyama wake aliyempotea, basi mwambie: “Allaah asikurudishie naye!” Misikiti haikujengwa kwa jambo hilo.”[1]

Je, mtu amwambie hivohivo anayeomba msikitini?

Jibu: Hapana. Mwombaji anaweza kuwa ni mwenye kuhitaji. Haina neno. Inafaa kwake kuomba akiwa ni muhitaji. Asiombewe du´aa mbaya. Lakini ukijua kuwa si mwenye kuhitaji,  basi mnasihi na umweleze kuwa haifai kwake kitendo hicho na kwamba ni haramu.

[1] Muslim (568).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 05/03/2022