Swali: Kuna wanaosema kuwa Imaam Muslim (Rahimahu Allaah) amekijenga kitabu chake juu ya kasoro, ya kwamba ametanguliza Hadiyth mbele wakati ilitakikana kuja nyuma, au kinyume chake, kutokamana na kasoro ndani yake na kwamba amezipangilia Hadiyth zake katika kitabu “as-Swahiyh” juu ya kasoro. Je, ni sahihi?

Jibu: Sijui mambo haya. Nani aliyesema hivo?

Muulizaji: Ni al-Miliybaariy. Ni muhindi mmoja aliyekuwa akisoma…

Jibu: Muhindi.

Muulizaji: Ndio. Dr. Hamzah al-Miliybaariy.

Swali: Ndio, huyu anajulikana. Shaykh Rabiy´ amemraddi mtu huyu. Mpigie simu Shaykh Rabiy´ na umuulize juu ya mtu huyo. Amemraddi kuhusiana na mambo haya.

Swali: Unaonaje juu ya Radd ya Shaykh Rabiy´ kwa mtu huyu? Je, ni Radd ni kielimu na yenye nguvu?

Jibu: Ndio ni ya kielimu. Inahusiana na Muslim. Amelidurusu suala hili. Vilevile ana kitabu kinachoitwa “Bayn al-Imaamayn ad-Daaraqutwniy wa Muslim”.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=155136
  • Imechapishwa: 28/07/2020