Ubora wa Maswahabah kwa njia ya jumla uko ifuatavyo:

1- al-Muhaajiruun ndio Maswahabah bora.

2- al-Answaar.

3- Walioshuhudia kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti.

4- Waliosilimu kabla ya kutekwa Makkah.

5- Waliosilimu baada ya hapo.

Amesema (´Azza wa Jall):

لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

“Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baada [ya ushindi] na wakapigana – na wote Allaah Amewaahidi Pepo. Na Allaah kwa yote myatendayo ni Mwenye khabari.” (57:10)

Makusudio ya “al-Fath” ni suluhu ya Hudaybiyah. Hawako sawa wale ambao walitoa kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti na wale waliosilimu baada ya hapo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 144
  • Imechapishwa: 27/08/2020