Mlinganizi anatakiwa kuwa msitari wa kwanza

Miongoni mwa adabu za kuamrisha mema na kukataza maovu (na hii sio sharti miongoni mwa masharti ya kuamrisha mema na kukataza maovu) ni yule anayefanya hivo awe mstari wa kwanza kufanya mema na awe msitari wa kwanza vilevile kuepuka maovu. Kwa msemo mwingine asiamrishe mema kisha yeye mwenyewe asiyafanye au akakataza maovu kisha akawe ni mwenye kuyafanya. Hili linaingia katika Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ

“Enyi walioamini!  Kwanini mnasema yale msiyoyafanya? Ni chukizo kubwa kabisa mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya!” (61:2-3)

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/358)
  • Imechapishwa: 08/01/2025