Mlee mtoto na kumtengeneza akiwa bado mdogo

Swali: Wakati fulani mwanangu ananitukana na wakati mwingine haswali. Nimeshindwa namna ya kutaamiliana naye. Je, nimuombe du´aa mbaya pamoja na kuzingatia kwamba ananambia kama nataka kuomba dhidi yake basi niombe nitakacho. Unatunasihi nini?

Jibu: Ndugu! Wazazi wengi wanawapuuza watoto wao. Hawawalei. [Sauti haiko wazi]. Wanasubiri mpaka pale wameshakuwa wakubwa. Hili ni kosa. Ulichotakiwa ni kumlea na kumtengeneza kuanzia mwanzo na kumpa malezi kutokana na dini na kumwamrisha kuhifadhi swalah:

“Waamrisheni watoto wenu kuswali wanapokuwa na miaka saba na wapigeni kwayo wanapokuwa na miaka kumi na watenganisheni katika malazi.”[1]

Ama kusubiri mpaka wameshakuwa wakubwa ni vigumu. Hutoweza. Lakini ungemlea tangu mwanzoni na ukawa naye, basi Allaah (´Azza wa Jall) angelimwongoza. Kwa sababu umefanya unachotakiwa kufanya.

Usimuombee du´aa mbaya. Mwombee kwa Allaah amwongoze. Allaah yukaribu na Mwenye kuitikia. Mwombee kwa Allaah amwongoze badala ya kumuombea du´aa mbaya.

[1] Ahmad na Abu Daawuud.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 03/04/2023