Swali: Mume akimpa pesa mmoja katika wakeze kama vile zawadi, analazimika kumpa yule mke mwingine?

Jibu: Kinachomlazimu ni yeye kumpa kila mwanamke haki yake. Kinachomlazimi ni yeye kuwahudumia, kuwapa kile wanachohitajia katika nguo, kuwapa makazi yanayoendana nao na kuwagawanyia siku za kulala. Hili ndio jambo la wajibu kwake.

Kuhusu zawadi, haimlazimu kuwagawanyia kiadilifu isipokuwa akichelea kutokea fitina na shari. Ima asimpe au akawapa wote wawili kwa kuepuka kusitokee fitina kati yao. Hafanyi hivo kwa njia ya kwamba ni lazima, isipokuwa ni kwa sababu ya kuepuka fitina na wivu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 04/04/2023