Mama mgonjwa wa akili na viungo ameacha swalah miaka mitatu

Swali: Mama yangu amesibiwa na maradhi ya viungo na ya kiakili. Hivi sasa haswali. Lakini si kwamba anashindwa kufanya hivo. Imempitia miaka mitatu akiwa katika hali hiyo na wala hafungi Ramadhaan. Je, tumtolee kafara ya swawm juu ya miaka mitatu iliyopita. Ni kipi kinachotupasa juu yake?

Jibu: Akiwa hana akili ´ibaadah si zenye kumuwajibikia. Kwa sababu hana akili na akili yake imechanganyikiwa. ´Ibaadah si zenye kumuwajibikia. Lakini akiwa bado yuko na akili basi haijuzu kwake kuacha swalah. Bali anatakiwa kuswali kutegemea hali yake na asiache swalah. Haitoshi kumtolea chakula. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah na achunge swalah. Allaah anamsamehe mwenye kutubia. Kwa sababu aliacha swalah kwa makusudi. Ambaye aliacha swalah kwa makusudi hailipi. Anachotakiwa ni yeye kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kulipa swalah kunakuwa kwa ambaye ameacha kwa kusahau au kwa kupitiwa na usingizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 03/04/2023