Mke wa kiyahudi au kinaswara katika kisiwa cha kiarabu

Swali: Muislamu ambaye anaye mke myahudi au mnaswara amwingize kisiwa cha kiarabu?

Jibu: Kinachodhihiri – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba haifai kwake kufanya hivo. Hilo linafanyika kama sio katika kisiwa cha kiarabu kama vile Shaam, ´Iraaq, Misri na kadhalika. Kwa sababu Hadiyth ni yenye kuenea:

“Watoeni mayahudi na manaswara nje ya kisiwa cha kiarabu.”[1]

Inamkusanya mke muislamu na mwengine.

[1] al-Bukhaariy (3053), Muslim (163), Abu Daawuud (3029) na Ahmad (1691). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

al-Fawzaan amesema:

“Hii ni kazi maalum inayomuhusu mtawala wa waislamu. Haijuzu kwa yeyote kuwaondoa, kama wanavoonelea hii leo wajinga katika vijana na wale walioathirika na maoni ya Khawaarij. Matokeo yake wakawa wanawaua wale walioahidiwa usalama na waliopewa mkataba wa amani, wanalipua majengo ambayo hawa makafiri walioahidiwa usalama na waliopewa mkataba wa amani wanaishi ndani yake. Hivyo wakawa wanafanya usaliti dhimma ya waislamu na wanakhaini ahadi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumuua aliyepewa mkataba basi hatonusa harufu ya Pepo.” (Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 90-92)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23616/حكم-ادخال-الزوجة-الكتابية-جزيرة-العرب
  • Imechapishwa: 29/02/2024