Swali: Je, ni Sunnah kuswali Rak´ah mbili hizi alizoswali Khubayb kabla ya kufa kwake?

Jibu: Hapana shaka kwamba zinapendeza. Anamalizia maisha yake kwa swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuzipinga na haikutufikia kuwa alizipinga. Khubayb aliziswali na zikatangaa.

Swali: Anayeuliwa kwa dhuluma?

Jibu: Ni vizuri akiwahi kuswali Rak´ah mbili. Anayamaliza maisha yake kwa swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23614/حكم-الركعتين-اللتين-صلاهما-خبيب-قبل-موته
  • Imechapishwa: 29/02/2024