Swali: Mwenye kuacha kutoa zakaah, swawm na hajj licha ya kwamba anakubali kuwa ni wajibu.

Jibu: Anakuwa mtenda dhambi na hakufuru. Bali anakuwa chini ya matashi ya Allaah, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth inayosema kuwa asiyetoa zakaah siku ya Qiyaamah ataadhibiwa kwa mali yake kisha baada ya hapo ataona nji yake ima ya kuelekea Peponi au ya kuelekea Motoni. Hilo ni tofauti na asiyeswali ambaye anakufuru hata kama hatokanusha uwajibu wake.

Swali: Vipi Abu Bakr kuwaua wasiotoa zakaah?

Jibu: Kwa sababu ya kuritadi kwao, kwa sababu waliritadi, wakaikanusha na wakakataa kumpa nayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23613/حكم-ترك-الزكاة-والصوم-والحج-دون-انكارها
  • Imechapishwa: 29/02/2024