76. Haijuzu kwa mfungaji kutumia vifunguzi vilivyotajwa

Ni haramu kwa mfungaji kutumia vifunguzi hivi ikiwa swawm yake ni ya lazima, kama vile swawm ya Ramadhaan, swawm ya kafara na swawm ya nadhiri, isipokuwa akiwa yuko na udhuru unaomruhusu yeye kufungua ikiwa ni pamoja na safari, maradhi na mfano wake. Kwa sababu atakayeanza kufanya jambo la wajibu analazimika kulikamilisha isipokuwa kukuwepo na udhuru sahihi.

Ambaye atafanya kifunguzi mchana wa Ramadhaan, pasi na udhuru, basi atalazimika kujizuia siku iliyobakia na baadaye alipe. Vinginevyo kama ni kutokana na udhuru atalazimika kulipa na si kujizuia.

Lakini ikiwa swawm yake ni ya kujitolea inafaa kwake kufungua hata kama ni pasi na udhuru ijapo bora ni kuikamilisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 102
  • Imechapishwa: 29/02/2024