Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anaenda na mke wake kwa walii ili aweze kushika mimba. Hivi sasa kila mwaka anamtembelea walii huyo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Akiona kuwa walii ndiye sababu ya yeye kushika mimba, ilihali amekwishakufa, anazingatiwa ni mshirikina. Akiona kuwa kama asingelienda kwa walii basi asingeshika mimba, basi vivyo hivyo anazingatiwa ni mshirikina. Ninachotaka kusema ni kwamba huu ni ukhurafi ambao ni lazima kwa waislamu kujiepusha nao:

هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّـهِ

”Je, kuna muumbaji mwingine badala ya Allaah?”[1]

Ni nani aliyekuumba kutokana na maji dhalili? Ni nani aliyekuumba wewe, mtoto wako, baba yako na babu yako?

[1] 35:3

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 26
  • Imechapishwa: 07/02/2025