Kufupisha swalah nyumbani kwa wazazi

Swali: Vipi kuhusu ambaye anawatembelea wazazi wake nyumbani kwao kwa siku mbili au tatu?

Jibu: Ikiwa anawatembelea na akasafiri, apunguze swalah hata kama anawatembelea wazazi wake. Lakini asiswali peke yake, anaswali pamoja na watu. Swalah ya mkusanyiko ni wajibu na kufupisha swalah ni Sunnah. Hivyo akiwa na ndugu yake, haijuzu kwake kuswali peke yake. Aswali na mkusanyiko na aswali kikamilifu. Lakini hapana vibaya akiwa na ndugu yake na wakapunguza swalah pamoja. Hata hivyo wataswali kikamilifu iwapo wanaswali na mkusanyiko.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25150/هل-يقصر-الصلاة-من-سافر-لزيارة-لوالديه
  • Imechapishwa: 07/02/2025