Tunaepuka mijadala. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna watu waliopotea baada ya uongofu waliyokuwemo isipokuwa baada ya kuanza kuleta mijadala.”

Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasoma Aayah ifuatayo:

مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ

”Hawakukupigia mfano huo isipokuwa tu kutaka kubisha. Bali wao ni watu makhasimu!”[1][2]

Mabishano yasiyo na manufaa ni yenye kusimangwa. Sisi hatukuwafukuza wala hatukutengana na ndugu isipokuwa ni kutokana na mambo ya uvyamavyama. Hatukutengana nao kwa sababu ya manufaa ya kidunia wala hatukutengana nao ili tuwe viongozi juu yao; tumefarikiana nao kwa ajili ya mambo ya uvyamavyama.

[1] 43:58

[2] at-Tirmidhiy (3253) na Ibn Maajah (48). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (141).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 143
  • Imechapishwa: 07/02/2025