Mitume na mashahidi wako hai ndani ya makaburi?

Swali: Je, ni kweli kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yuko hai ndani ya kaburi lake?

Jibu: Ndio, yuhai uhai wa maisha ya ndani ya kaburi. Allaah ameeleza kwamba mashahidi pia wako hai. Lakini hata hivyo inahusiana na maisha ya ndani ya kaburi na sio kama maisha waliokuwa nayo duniani. Ni maisha ya ndani ya kaburi. Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) ni wakubwa zaidi kuliko mashahidi. Wao wako na haki zaidi ya kuwa hai ndani ya makaburi yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (93) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighstah%20-20-1-1440_0.mp3
  • Imechapishwa: 20/04/2019