11. Kufunga swawm zilizopendekezwa kabla ya kulipa Ramadhaan

Swali 11: Ni ipi hukumu ya swawm iliyopendekezwa kama mfano wa zile siku sita za Shawwaal, zile siku kumi za Dhul-Hijjah na siku ya ´Aashuuraa´ kwa yule ambaye anadaiwa baadhi ya siku za Ramadhaan?

Jibu: Kwa yule ambaye analazimika kulipa deni lake la Ramadhaan ni lazima kwake aanze kulilipa kabla ya swawm ya Sunnah. Kwa sababu faradhi ni muhimu zaidi kuliko ´ibaadah iliyopendekezwa. Haya ndio maoni yenye nguvu zaidi ya wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 19
  • Imechapishwa: 20/04/2019