Swalah ya kupatwa kwa jua katika nchi ya kikafiri

Swali: Umetaja kwamba swalah ya kupatwa kwa jua ni swalah ya khofu kutokana na adhabu ya Allaah ambayo inaswaliwa ili Allaah awaondoshee watu adhabu. Katika miji ya makafiri wanaishi baadhi ya waislamu. Je, hilo likitokea kwao ni wajibu kwa watu hawa kuiswali?

Jibu: Ndio. Ni wajibu kwa waislamu kila mahali waswali kupatwa kwa jua. Lakini ni kama nilivosema tokea mwanzo kwamba ni faradhi kwa baadhi ya watu. Adhabu ya Allaah (´Azza wa Jall) ikiteremka ni yenye kuenea kwa mwema na asiyekuwa mwema na kila mmoja siku ya Qiyaamah atafufuliwa juu ya nia na matendo yake. Usisemi kuwa huu ni mji wa kikafiri. Hata kama ni nchi ya kikafiri inatakiwa kuswali swalah ya kupatwa kwa jua. Ni kama ambavyo unaswali zile swalah tano.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1115
  • Imechapishwa: 20/04/2019