Nimepata swali lako linalohusu kukata baadhi ya nywele na kuacha zingine. Jawabu ni kama ifuatavyo:

Himdi zote njema anastahiki Allaah. Abu Daawuud amepokea kwamba ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtoto amekata baadhi ya nywele na kuacha zingine na akasema: “Ima zinyoe zote au ziache zote.”

al-Bahuutiy amesema katika “Sharh-ul-Iqnaa´”:

“Miongoni mwa mitindo hiyo kunaingia vilevile kunyoa sehemu za pembeni ya kichwa, au akanyoa sehemu ya katikati yake na akaacha sehemu za pembeni, kama wanavofanya manaswara wengi, au kunyoa sehemu za pembeni na kuacha sehemu za katikati, kama wanavofanya wapumbavu wengi, au akanyoa sehemu ya mbele na akaacha sehemu ya nyuma. Ahmad ameulizwa kuhusu kunyoa sehemu ya shingo ambapo akasema: “Ni katika mambo ya waabudia moto; yeyote mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Kutokana na tuliyoyataja inabainika kuwa mitindo hiyo haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (2/42-43)
  • Imechapishwa: 23/03/2024