Muhammad bin Ibraahiym Aal ash-Shaykh kuhusu Saudi Arabia

Katiba ya Saudi Arabia – na himdi zote njema anastahiki Allaah – ni Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili hiyo kumefunguliwa mahakama ya Shari´ah kwa ajili kuhakikisha maneno Yake Allaah (Ta´ala):

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.”[1]

Yasiyokuwa hayo ni katika hukumu za kipindi kabla ya kuja Uislamu. Amesema (Ta´ala):

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ

“Je, wanataka hukumu za kipindi cha kijahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.”[2]

[1] 4:59

[2] 5:50

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/288)
  • Imechapishwa: 23/03/2024