Muhammad bin Ibraahiym kuhusu al-Albaaniy na mwanamke kujipamba kwa dhahabu

Baadhi ya watu wanaona kuwa haijuzu kwa mwanamke kujipamba na dhahabu na wakaandika juu ya mada hiyo. Jambo hili linapingana na Hadiyth ambazo zimetaja waziwazi kufaa kwa jambo hilo. Ambaye ameandika juu ya hilo ni [Muhammad] Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Ni mtu ambaye anashikamana barabara na Sunnah, kuinusuru haki na kukabiliana na watu wa batili. Hata hivyo yuko na baadhi ya maoni dhaifu na hili ni moja wapo. Haonelei kufaa kutumia dhahabu na amejengea hoja na kukusanya mapokezi kadhaa, lakini hayawezi kuzipinga Hadiyth.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (4/92)
  • Imechapishwa: 23/03/2024