al-´Adawiy alikuwa ni katika Ahl-us-Sunnah

Swali: Je, Mustwafaa al-´Adawiy ni katika Ahl-us-Sunnah?

Jibu: Alikuwa ni katika Ahl-us-Sunnah. Kisha akaanza kuchanganyika na baadhi ya Hizbiyyuun na ndipo akaathirika nao. Nimemzungumzia Mustwafaa al-´Adawiy na kusema kwamba alikuwa ni katika Ahl-us-Sunnah kisha akapondoka kitu katika upindaji.

Kuhusu vitabu vyake vyenye manufaa kama vile “al-Adhkaar” ambacho ameandika wakati alipokuwa kwa Shaykh Muqbil, watu wanufaike navyo. Kuhusu vitabu vyake alivyoandika Misri na ambavyo viko na makosa na upindaji, watu waviepuke. Wanazuoni pekee ndio wanaotakiwa kuvisoma.

Moja katika makosa aliyotumbukiaemo ni kumtukana Shaykh al-Albaaniy. Allaah amejaalia Shaykh Ahmad bin Abiyl-´Aynayn akamraddi[1]. Yeye pia ni mmisri na ni mkwe wake. Amemraddi Mustwafaa al-´Adawiy katika vitabu vingi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kuanzia-katika-kumraddi-mustwafaa-al-adawiy-na-kwenda-katika-mfumo-wake-imekuweje/

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://olamayemen.com/Dars-13758
  • Imechapishwa: 23/03/2024