Kuanzia katika kumraddi Mustwafaa al-´Adawiy na kwenda katika mfumo wake – imekuweje?

Swali: Siku chache zilizopita, Ahmad bin Abiyl-‘Aynayn wa Misri, mkwe wa Mustwafaa al-‘Adawiy na mwanafunzi wa Shaykh Muqbil, alichapisha kitabu ambamo anajuzisha ndani yake maandamano na kufaa kufanya uasi dhidi ya watawala madhalimu na amewatukana wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah. Kitabu hicho kinaitwa “al-Kawaashif al-Jalliyyah fiy Hukm at-Thawraat al-‘Arabiyyah”. Tungependa Shaykh aliraddi jambo hili kwani mambo kama haya yanaweza kuwachanganya vijana wa ki-Salafiy.

Jibu: Ahmad bin Abiyl-‘Aynayn hakupata jambo hilo kutoka kwa Shaykh Muqbil. Amepata jambo hilo wakati alipochanganyika na Khawaarij wa Misri. Mimi namshauri atubie kwa Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na Bid´ah za Khawaarij na arudi kwa yale aliyokuwemo hapo kabla katika kujifunza elimu na kuielewa dini na kushikamana barabara na Qur-aan na Sunnah. Anapaswa kujua kuwa hivi sasa anafuata njia isiyokuwa ya mwalimu wake Shaykh Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy na njia isiyokuwa ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambayo wanaifata miaka yote. Anafuata njia ya Khawaarij. Asipojirejea hamdhuru yeyote isipokuwa nafsi yake na wala hamdhuru Allaah chochote. Dini ya Allaah imehifadhiwa. Kundi lililonusuriwa litaendelea kuwepo juu ya haki. Ni juu yake kujiepusha kuketi na Khawaarij hata kama watajidai kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah. Wao sio katika Ahl-us-Sunnah. Wao ni wazushi. Katika jambo hili wao ni katika Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´.

Ee Ahmad! Ulikuwa na tungo na vitabu vizuri. Nilikuwa navipenda na kuvisoma mpaka nilipofikiwa na khabari kwamba umebadilika. Tunamuomba Allaah akuthibitishe wewe, sisi na waislamu wote juu ya Qur-aan na Sunnah.

Fanya haraka kujirejea katika mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kujiweka mbali na Khawaarij. Tubu kwa Allaah kutokana na makosa ulioingia ya ´Aqiydah, ya mfumo na ya ulinganizi katika vitabu vyako hivi vya mwisho.

Yule anayejichanganya na Ahl-ul-Bid´ah wanamdhuru na kumtia sumu. Kwa ajili hiyo mfumo wa Salaf ni kujiweka mbali na kuketi na Ahl-ul-Bid´ah na kutoongeza wingi wao. Huu ndio mfumo sahihi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ

”Unapowaona wale wanaoziingilia na kuzishambulia Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu madhalimu.” (06:68)

Allaah akuongoze! Sulikuwa ukimraddi Mustwafaa al-´Adawiy. Hivi sasa unapita mapito yake, mapito ya Qutbiyyuun, mapito ya Suruuriyyuun na mapito ya Khawaarij.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://youtu.be/N6k94BBZHFM?si=9CtX8_8JhJ22MvcJ
  • Imechapishwa: 23/03/2024