Miongoni mwa tiba za hasadi

Swali: Je, miongoni kwa tiba za hasadi ni mtu kusema:

اللهم زدنا وإياه

“Allaah Allaah! Tuzidishie sisi na yeye.”

au:

اللهم ارزقنا وإياه

“Ee Allaah! Turuzuku sisi na yeye.”?

Jibu:

بارك الله له

“Allaah ambariki.”

بارك الله فيه

“Allaah ambarikie.

ما شاء الله

“Yale aliyoyataka Allaah.”

Hivi ndio tiba:

وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ

“Na lau ulipoingia bustanini mwako ungelisema: ‘Ametaka Allaah, hapana nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah´.”[1]

Akiona jambo linalompendeza aseme:

بارك الله فيه

“Allaah ambarikie.”

مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ

”Ametaka Allaah, hapana nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Hivo ni katika tiba.

[1] 18:39

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23445/ما-المشروع-قوله-لاتقاء-الحسد
  • Imechapishwa: 24/01/2024