02. Hadiyth “Yule mwenye kusoma Suurah “al-Kahf” atakuwa na nuru mpaka siku ya Qiyaamah… “

225 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kusoma Suurah “al-Kahf” atakuwa na nuru mpaka siku ya Qiyaamah kutokea maeneo pake mpaka Makkah. Yule mwenye kusoma Aayah kumi za mwisho wake kisha akajitokeza ad-Dajjaal, hatomdhuru. Ambaye atatawadha na akasema:

سُبْحانَكَ اللهُمَّ وَبِحَمْدِكَ أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْكَ

“Kutakasika na mapungufu ni Kwako, ee Allaah, na himdi zote njema ni Zako. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe na nakuomba msamaha na kutubu Kwako.”

ataandikiwa nayo kwenye karatasi kisha baadaye itapigwa muhuri. Haitovunjwa mpaka siku ya Qiyaamah.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Tamko ni lake. Imekujna kwa an-Nasaa’iy:

خُتِم عليها بخاتَم فوضِعتْ تحتَ العرشِ، فلم تُكسَر إلى يومِ القيامةِ

“… kisha baadaye itapigwa muhuri na kuwekwa chini ya ´Arshi. Haitovunjwa mpaka siku ya Qiyaamah.”

Ameona kuwa sahihi zaidi ni maneno ya Abu Sa´iyd[2].

[1] Swahiyh.

[2] Lakini yana hukumu moja kama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu udhahiri ni kwamba jambo hilo halisemwi kutokana na maoni ya mtu mwenyewe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/209)
  • Imechapishwa: 24/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy