Usimsuse mke zaidi ya siku tatu

Swali: Je, inafaa kwa mume kumkata mke zaidi ya siku tatu katika jambo miongoni mwa mambo ya kidunia?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ

“Na wale ambao mnachelea uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni.”[1]

Hadiyth imefungamanisha kilichoachiwa. Ikiwa kumsusa ni kwa haki ni kwa muda wa siku tatu. Ikiwa ni kwa haki yake mtu au ni kwa maasi azidishe siku tatu.

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakata wakeze mwezi.

Jibu: Huku ni kuwasusa kwake wote. Kwa sababu walimwomba jambo ambalo si halali kwao, ni maasi yao.

[1] 04:34

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23444/حكم-هجر-الزوج-لزوجته-اكثر-من-ثلاثة-ايام
  • Imechapishwa: 24/01/2024