60. Athar ”Walikuwa wanapendekeza mtu kusema… ”

60 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia: Sa´iyd al-Jariyriy ametuhadithia, kutoka kwa Zayd bin ´Abdillaah, ambaye amesema:

”Walikuwa wanapendekeza mtu kusema:

اللهم صل على محمد  النَّبِيّ الأُمِّيّ

“Ee Allaah! Msifu Muhammad Mtume ambaye si msomi!”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh lakini imekatika. Zayd bin ´Abdillaah ni katika tabaka la wanafunzi wa Maswahabah. Katika tabaka hili alikuwepo Zayd bin ´Abdillaah bin ´Umar bin al-Khattwaab, kwa hivyo kuna uwezekano ndiye. Hata hivyo hakutajwa mpokezi yeyote kutoka kwa Sa´iyd al-Jariyriy. Kuna uwezkeano vilevile ikawa ni kosa cha uchapaji na inatakiwa iwe Yaziyd badala ya Zayd. Katika hali hiyo Yaziyd bin ´Abdillaah bin ash-Shukhayr al-´Aamir, ni mmoja katika wapokezi wa al-Jariyriy wanaotambulika – na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kisha nihakikisha uwezekano huu wa pili wakati nilipomuona Ibn-ul-Qayyim akinakili cheni hiyohiyo katika “Jalaa-ul-Afhaam”, uk. 76, kwa Yaziyd bin ´Abdillaah.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 24/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy