59. Hadiyth “Bwana mmoja alimjilia Mtume wa Allaah… “

59 – Ahmad bin ´Abdillaah bin Yuunus ametuhadithia: Zuhayr ametuhadithia: Muhammad bin Ishaaq ametuhadithia: Muhammad bin Ibraahiym bin al-Haarith ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Abdillaah bin Yaziyd, kutoka kwa ´Uqbah bin ´Amr, ambaye amesema:

“Bwana mmoja alimjilia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mpaka akaketi mbele yake na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Kuhusu kukutakia amani tumekwishajua, lakini unaweza kutueleza ni namna gani ya kukuswalia?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanyamaza mpaka tukatamani mtu aliyemuuliza asingemuuliza. Kisha akasema: “Mtaponiswalia, basi semeni:

اللهم صل على محمد  النَّبِيّ الأُمِّيّ و على آل محمد كما صليت على إبراهيم و آل إبراهيم. و بارك على محمد  النَّبِيّ الأُمِّيّ و على آل محمد كما باركت على إبراهيم وآل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad Mtume ambaye si msomi na jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Na mbariki Muhammad Mtume ambaye si msomi na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni nzuri. Ameipokea  Abu Daawuud (981), Ibn Abiy Shaybah (2/508), Ibn Hibbaan (510), ad-Daaraqutwniy, uk. 135-136, al-Haakim (1/268) na al-Bayhaqiy (2/146-147) kupitia njia nyingine, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq. ad-Daaraqutwniy amesema kuwa ”cheni ya wapokezi ni nzuri na ni yenye kuungana”. al-Haakim amesema kuwa cheni ya wapokezi ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 58
  • Imechapishwa: 24/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy