58. Hadiyth ”Ee Mtume wa Allaah! Hakika tumejua namna ya kukutakia amani… ”

58 – Musaddad ametuhadithia: Abul-Ahwas ametuhadithia: Yaziyd bin Abiy Ziyaad ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Ka´b bin ´Ujrah, ambaye amesema:

”Ee Mtume wa Allaah! Hakika tumejua namna ya kukutakia amani, tunakuswalia namna gani?” Akasema: ”Semeni:

اللهم صل على محمد و على آل محمد كما صليت على إبراهيم و آل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[1]

[1] Imekuja namna hii katika ile ya asili, pasi na kuombewa baraka. Hata hivyo ni jambo limethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim na wengineo, kwa tamko lisemalo:

اللهم بارك على محمد و على آل محمد كما باركت على إبراهيم إنك حميد مجيد

”Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhimidiwa na Mwenye kutukuzwa.”

Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Wote wawili wameipokea kwa njia nyngi kutoka kwa Shu´bah.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 57
  • Imechapishwa: 24/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy