Swali: Je, imekatazwa kwa mtu kusema kuwa ni Maalikiy au Hanbaliy? Baadhi ya wanafunzi wanasema kuwa haifai kusema hivo.

Jibu: Anataka aseme nini? Hakuna kosa kwa mtu kusema kuwa ni Hanbaliy, Shaafi´iy, Maalikiy… Haya ni madhehebu ya Ahl-us-Sunnah. Je, unapinga madhehebu ya Ahl-us-Sunnah? Haijuzu. Hata hivyo hutakiwi kusema kuwa haki iko tu katika madhehebu ya Hanaabilah. Haijuzu. Ama kusema kuwa madhehebu yote mane ni ya Ahl-us-Sunnah, ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331116.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015