Usiwaache watoto zako wakaenda sehemu za TV

Swali: Kuna mtu hawakatazi watoto wake kutazama TV wakati wanapokuwa kwa ndugu zao. Hata hivyo amekataa kuingiza TV nyumbani kwake ili aweze kuwalea, awakuze kidini na kuwafanya wasome vitabu pasina ya wao kutambua hilo. Amefanya sawa?

Jibu: Wakitazama TV kwa wengine, watakuja kuiomba nyumbani pia. Watatoa amri; ima ulete TV au tunatoka na kwenda kwenye nyumba ya jirani au mtu mwingine ambaye yuko na TV. Usiwaache wakaenda kwenye nyumba zilizo na TV. Ikiwa kweli unataka kuwalea vizuri, usiwaache wakaenda huko.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331116.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015