Kuwalea watoto kunahitajia mapambano na nguvu

Swali: Tukiwakataza watoto wetu wa leo na vyombo vya khabari, wataenda kwa wengine. Tufanye nini?

Jibu: Umesikia jibu.[1] Wakataze. Ni wadogo. Wataacha. Wakatazae wakati ni watoto. Hawatoenda. Hili linahitajia kupambana nao na kuwa na subira kwao. Linahitajia uangalizi na uchungaji na kutochukulia usahali. Ukiwaacha watoto zako wakaenda kwa majirani na ndugu wasiokuwa na dini, bila ya shaka wataathirika na hapo itakuwa vigumu kwako kuwaelekeza. Kuwakataza inahitajia subira na nguvu na kuwepo. Kwa kuwa baadhi ya wazazi hawapo nyumbani. Hawaji nyumbani isipokuwa wamechelewa na usiku. Haulizi watoto wake na wala yaliyopitika nyumbani. Haya, pamoja na kwamba yeye ndiye mchungaji nyumbani:

“Nyote ni wachungaji na kila mmoja ataulizwa kwa kile alichochungishwa.”

Mwanaume nyumbani ni mchungaji na ataulizwa juu ya kile alichochungishwa.

———–

(1) Tazama https://firqatunnajia.com/usiwaache-watoto-zako-wakaenda-sehemu-za-tv/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331116.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015