Swali: Nina baadhi ya marafiki zangu wanaoenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ninakaa pamoja nao na wakati mwingine ninawaita katika duruus ya ´Aqiydah kwa sababu mimi mwenyewe siwezi kuwanasihi. Je, ni sahihi kwangu kukaa nao na kuwaita katika duruus ya ´Aqiydah?

Jibu: Ikiwa wanaoenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wewe unatangamana nao kwa ajili ya kuwanasihi na kuwafunza kwa sababu pengine wakawa ni wajinga, ni jambo zuri. Ama ikiwa unatangamana nao na shari zao kwa ajili ya kufurahi nao na sio kwa ajili ya kuwalingania, hili halijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-5-11-1435.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015