Bay´ah ya kuzushwa inawagawa waislamu zaidi na zaidi

Swali: Ni ipi hukumu ya kumpa bay´ah kiongozi wa kundi ikiwa hajulikani kwa elimu? Kwa mfano al-Ikhwaan al-Muslimuun wanampa bay´ah kiongozi wao na wakati mwingine inatokea anakuwa ni mjinga. Ni ipi hukumu ya bay´ah kama hizi?

Jibu: Hili ni tatizo jengine. Miaka yote iliyopita waislamu hawatambui mtu yeyote ya kwamba anapewa bay´ah isipokuwa kiongozi wa waislamu. Lakini kwa masikitiko makubwa wakati mapote yalipokuwa mengi wakazidi kwenda mbali zaidi na Uislamu na kuwalazimisha wafuasi wao kuwapa bay´ah. Kutokana na bay´ah hizo wana hukumu ambazo si sahihi kupewa mtu yeyote isipokuwa Khaliyfah wa waislamu.

Lililo la ajabu ni kwamba watu hawa wanafuata matamanio yao na wanatendea kazi hukumu za Kishari´ah zile ambazo zinaenda sambamba na mifumo yao ambayo wamepinda kwayo katika Qur-aan na Sunnah. Kuna Hadiyth inayosema:

“Wakipewa bay´ah makhaliyfah wawili basi muueni yule wa mwisho.”

Hawaijali kabisa Hadiyth hii. Kwa sababu ina maana kila yule anayepewa bay´ah, ni lazima kuwepo ambaye tayari alikuwa ameshapewa bay´ah wakati yule anayejigawa naye auawe ili kusiwepo fitina yoyote. Kwa ajili hiyo ndio maana bay´ah hapewi isipokuwa mtu mmoja tu. Kwa kuzingatia ya kwamba mtu kama huyu hayupo katika kipindi hichi cha mwisho kuna watu ambao wanataka kushikilia kitu walichokikosa. Lakini wanafanya hivo kwa njia inayoenda kinyume na Shari´ah. Hivyo basi ni wajibu kwa waislamu kutojigawa mapote na makundi. Na wakigawanyika haitakiwi kuongeza mgawanyiko huu ili kujengea juu yake baadhi ya hukumu. Mtindo kama huu unaokubaliana na mgawanyiko huu unasababisha tu Waislamu kuzidi kugawanyika zaidi na zaidi. Mola Wetu (´Azza wa Jall) Ametukataza hili wakati Aliposema:

مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَاتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

“[Shikamaneni nayo dini ya Kiislamu na mbakie daima humo] wenye kurudi kutubu Kwake na mcheni, na simamisheni swalah; na wala msiwe miongoni mwa washirikina. Miongoni mwa wale walioitenganisha dini yaowakawa makundi makundi. Kila kundi kwa yaliyonayo linafurahia.” (30:31-32)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (26)
  • Imechapishwa: 19/04/2015