Mgonjwa aliyechelewesha kulipa deni lake la Ramadhaan baada ya kupona

Kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym kwenda kwa muheshimiwa X.

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Barua yako imetufikia ambapo unauliza kinachokulazimu kwa vile hukuweza kufunga Ramadhaan ya mwaka wa 1374 hadi sasa kwa sababu ya ulipatwa maumvu ya mgongo na kupooza kwa miguu na kwamba ulijaaliwa kufunga Ramadhaan ya mwaka wa 1385.

Jawabu ni kwamba kufunga Ramadhaan ya mwaka wa 1384 bado kunakulazimu mpaka sasa. Amesema (Ta´ala):

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

”Atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.” (02:185)

Isitoshe kwa sasa umepona. Kwa hivyo ni wajibu kwako kulipa mwaka huo pale utapoweza kutokana na Aayah iliyotangulia.

Kuhusu kuchelewesha mwaka wa 85 na mwaka wa 86, ikiwa kipindi hicho ulikuwa unaweza kulipa, basi utalazimika vilevile kumlisha chakula masikini kwa kila siku moja iliyokupita. Hilo ni kwa mujibu wa maoni ya Ibn ´Abbaas, Ibn ´Umar na Abu Hurayrah. Ndio maoni vilevile ya Maalik, Ahmad na ash-Shaafi´iy. Na kama si muweza basi haikulazimu. Amesema (Ta´ala):

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)

Muftiy wa Saudi Arabia

16/10/1386

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (200-201)
  • Imechapishwa: 24/03/2024