Mgeni ni wajibu kumuuliza Qiblah mwenyeji

Ni wajibu kwa mgeni anapofika kwa mwenyeji wake na akataka kuswali Sunnah amuulize Qiblah kilipo. Akimwambia kilipo akielekee. Baadhi ya watu wanaona hayaa na hapa haya sio mahali pake. Kuuliza Qiblah kilipo ni hayaa isiyokuwa mahali pake. Baadhi ya watu wanaona hayaa kuuliza Qiblah kilipo ili watu wasisemi ya kuwa hajui. Haidhuru kitu. Aseme anachotaka. Linalompasa ni yeye aulize mahali Qiblah kilipo ili mwenyeji akueleze. Kuna watu wanaona hayaa na hilo linampelekea  kujitahidi mwenyewe kuelekea upande fulani na [baadaye] inambainikia kuwa alielekea makosa, katika hali hii ni wajibu kwake kurudi swalah yake kwa sababu ameegemea katika jambo ambalo halikuwekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/376)
  • Imechapishwa: 23/05/2023