Watu wa vituko wanaomjulisha Allaah nia zao

Kuna mtu (Rahimahu Allaah) alinieleza kisa. Kuna bwana mmoja kwenye msikiti Mtakatifu hapo kitambo alitaka kuswali baada ya kukimiwa swalah. Akasema “Ee Allaah! Hakika mimi nanuia kuswali Dhuhr Rak’ah nne kwa ajili Yako (Ta´ala), nyuma ya imamu wa msikiti Mtakatifu”. Alipotaka kusema “Allaahu Akbar” kuna mtu alikuwepo pambizoni mwake akamwambia “Subiri, kuna kitu umesahau.” Akauliza “Nimesahau nini?”. Akamwambia “Umesahau kutaja ni siku gani, tarehe gani na mwaka gani” ili yasije yakapotea [matendo yako]. Yule mtu akashangaa. Na ni kweli ni kitu kinachoshangaza. Je, wewe unamuelimisha Allaah (´Azza wa Jall) unachokusudia? Allaah anajua yanayopitika katika nafsi. Je, wamweleza Allaah kuwa unaswali Rak’ah nne na wakati? Hakuna haja ya hili. Allaah anajua hili. Nia mahali pake ni moyoni.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/378)
  • Imechapishwa: 23/05/2023