Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak na dawa ya meno mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Kutumia Siwaak[1] hapana vibaya. Haijalishi kitu hata kama ni wa kijani. Kuhusu dawa ya meno tunashauri kuiepuka katika Ramadhaan. Hatuna dalili inayoonyesha kuwa inaharibu swawm. Hata hivyo ni wajibu kwa mtu kuwa makini ili kusiingie kitu tumboni mwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fanya kishindo katika kuyapindisha maji puani isipokuwa ukiwa umefunga.”

Kwa sababu ikiwa amefunga kuna khatari maji yakaingia tumboni mwake.

[1] Tazama https://sw.wikipedia.org/wiki/Mswaki_(mti)

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 78-79
  • Imechapishwa: 16/03/2024