Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke ambaye amepata hedhi muda mfupi tu kabla ya kufungua?

Jibu: Analazimika kuilipa siku hiyo ikiwa muadhini anaadhini ndani ya wakati. Lakini kama amepata hedhi baada ya jua kuzama na muadhini anaadhini baada ya kuingia usiku, kama wanavofanya Shiy´ah, swawm yake ni sahihi. Katika hali hiyo hatolazimika kulipa siku hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 77
  • Imechapishwa: 16/03/2024