Mfano wa Bid´ah nzuri ni kama ile aliyokusudia ´Umar

Swali: Je, miongoni mwa Bid´ah ipo Bid´ah nzuri kwa maana ya kilugha na sio kwa maana ya kiistilahi?

Jibu: Ni jambo linalotambulika kwamba Bid´ah zote ni upotevu, kama alivosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bid´ah ya kilugha yenye maana kwamba mtu akazusha kitu ambacho hakikujengeka juu ya msingi ni kama mfano wa ile aliyosema ´Umar, wakati alipoambiwa kuhusu swalah ya Tarawiyh, akasema:

“Neema ya Bid´ah hiyo.”

Tarawiyh sio Bid´ah. Kwa sababu kitendo cha ´Umar kuwakusanya watu katika Tarawiyh ni jambo lina msingi katika dini na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha watu katika Ramadhaan nyusiku tatu. Lakini akiache kuendelea kufanya hivo akabainisha sababu kwa kuchelea isije kufaradhishwa. Kwa hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaiacha kwa kuchelea isije kufaradhishwa kwa watu, jambo ambalo ni katika huruma, wema wake na upole wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Allaah awawie radhi Maswahabah wote. Lakini wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofariki na Shari´ah ikathibiti na kusimama usiku ikawa ni jambo lililopendekezwa na kitendo alichofanya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kikawa kimependekezwa na hakikufaradhishwa tena kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameshakufa, ndipo ´Umar akalifufua tena. Pindi alipoambiwa ndio akasema:

“Neema ya Bid´ah hiyo.”

Kwa hiyo anakusudia Bid´ah ya kilugha lakini hata hivyo msingi wake upo katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 09/11/2019